Kikao cha ufunguzi kimehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya, baadhi ya marais wa vitengo, viongozi mbalimbali na taasisi zinazojishughulisha na mambo ya kiteknolojia.
Kongamano la Multaqal-Kafeel linafanyika katika eneo la chuo kikuu cha Al-Ameed kuanzia tarehe (30/10 hadi 1/11/2023m), vitenge tofauti vya Atabatu Abbasiyya vinashiriki kuonyesha uzowefu wao katika sekta ya teknolojia.
Kongamano linavipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kubainisha mtazamo wa Atabatu Abbasiyya kufuatia maendeleo ya dunia.
Jumla ya vitengo saba vya Atabatu Abbasiyya vimeshiriki kwenye kongamano hilo na jumla ya jukwaa 18 za kielimu zimefafanuliwa.
Katika siku ya kwanza umetolewa utambulisho wa huduma zinazotolewa na jukwaa za kielimu, kongamano litadumu kwa muda wa siku tatu na linavipengele tofauti.