Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kinafanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wake.
Program hiyo imepewa jina la (Nani wewe) wakufunzi wa ratiba hiyo wamebobea katika elimu ya nasfi na utatuzi wa changamoto za kimaadili, wanaongozwa na Dokta Shaimaa Naasir.
Ratiba itadumu kwa muda wa mwezi mmoja, masomo yanatolewa siku mbili kwa wiki, washiriki wanafundishwa namna ya kutatua migogoro ya kifamilia na kimaadili sambamba na njia bora za kutumikia jamii kwa kufuata muongozo wa Ahlulbait (a.s).