Idara ya maelekezo ya Dini inaendelea na ratiba ya mafunzo ya (Najielekeza kwa Abulfadhil).

Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inaendesha mafunzo ya (Najielekeza kwa Abulfadhil) kwa watumishi wa idara ya Zainabiyaat.

Program imejikita katika kufundisha mbinu za kuamiliana na watu, sambamba na kujibu maswali kutoka kwa washiriki.

Masomo hayo yanatolewa siku mbili kwa wiki, ndani ya Sardabu ya Alqami katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ratiba hii ni sehemu ya kuwajengea uwezo wasichana wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: