Atabatu Abbasiyya imewapa zawadi washiriki wa kongamano la kiteknolojia Multaqal-Kafeel.

Atabatu Abbasiyya tukufu imewapa zawadi washiriki wa kongamano la Multaqal-Kafeel kwenye hafla ya kufunga kongamano hilo iliyofanyika leo.

Washiriki walio onyesha shughuli mbalimbali za kiteknolojia, kama vile App, toghuti na mambo mengine, kutoka vitengo tofauti vya Ataba wamepewa zawadi.

Wamemshukuru kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na uongozi mkuu, wakasema kuwa zawadi walizopewa zinawapa hamasa kubwa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi kwenye sekta ya teknolojia.

Kongamono limefanyika kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe (30/10/ hadi 1/11/2023m) katika eneo la chuo kikuu cha Al-Ameed, vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya vimeshiriki kuonyesha shughuli zao na uzowefu wao kwenye sekta ya teknolojia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: