Majmaa-Ilmi inafanya semina ya Qur’ani kwa wasomaji wa mkoa wa Muthanna.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya semina ya Qur’ani kwa wasomaji wa mkoa wa Muthanna.

Semina inasimamiwa na kituocha miradi ya Qur’ani kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’ani tukufu ya mkoani hapo.

Kwenye semina hiyo wanafundishwa hukumu za usomaji wa Qur’ani, sauti, naghma, njia za kurefusha usomaji pamoja na kufafanua utambulisho wa kitamaduni kwa mtu.

Wakufunzi wa semina hiyo ni walimu wa kituo (Ali Saaidi, Muhammad Ridhwa Zubaidi na Liith Ubaidi), kila siku hupangiwa mada maalum.

Kumbuka kuwa kituo cha miradi ya Qur’ani katika Majmaa-Ilmi, hufanya semina na warsha mbalimbali kwa kushirikiana na taasisi tofauti za Qur’ani kwenye miji tofauti ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: