Kitengo cha maarifa ya kiislam na kibinaadam katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa wito kwa watafiti wa kushiriki kuandika jarida la (turathi za kusini).
Jarida limejikita katika kuandika turathi za mikoa minne ambayo ni (Dhiqaar, Misaan, Qaadisiyya na Muthanna), zinahitajika tafiti za mambo yafuatayo (Dini, Adamu, lugha, viongozi na watu maarufu, maktaba za serikali na binafsi, majengo, malalo za waja wema, mazaru na mengineyo.
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kinajarida zingine tatu, ambazo ni {Jarida la turathi za Karbala, jarida la turathi za Basra na jarida la turathi za Hilla).