Kitengo cha mahusiano kinafanya kikao cha kwanza kujadili maandalizi ya hafla ya kuhitimu wanafunzi wa chuo.

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimefanya mkutano wa kwanza kujadili maandalizi ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq kikosi cha (Juu ya uongofu wa mwezi) awamu ya tatu.

Idara imefanya kikao cha maandalizi ya mahafali ya wahitimu, kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule Sayyid Maahir Khalidi amesema kuwa “Tumefanya kikao cha maandalizi ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu yatakayo fanywa chini ya jina la (Juu ya uongofu wa mwezi) awamu ya tatu”.

Akaongeza kuwa “Mkutano umejadili namna ya kugawa majukumu kulingana na vitengo, aidha yakajadiliwa pia mambo ya kiutawala, ikiwa ni pamoja na usafiri, chakula, zawadi na kipengele cha uwasilishaji wa tafiti mbalimbali”.

Mahafali inatarajiwa kuhudhuriwa na wahitimu wa vyuo tofauti vya Iraq kutoka mikoa mbalimbali, kaskazini, kusini na ukanda wa kati, wahitimu wanaotarajiwa kushiriki ni zaidi ya 2500 kwa mujibu wa maelezo ya Khalidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: