Kitengo cha maarifa kimepokea wageni kutoka chama cha waandishi wa Habari wa kiiraq katika mji wa Baabil.

Kitengo cha maarifa ya kiislam na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimepokea ugeni kutoka chama cha waandishi wa Habari wa kiiraq tawi la Baabil.

Ugeni huo unaongozwa na rais wa chama hicho Sayyid Yusufu Abdu-Auni Aljamalu, wamepokewa na mkuu wa kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha Shekhe Swadiq Khuwailidi.

Wageni wameangalia matokeo ya kielimu na kimaarifa yaliyofikiwa na kituo, nafasi yake kwenye vyombo vya Habari kupitia yanayo tangazwa na kuandikwa, wakapongeza jarida linalotolewa na kituo cha maarifa ya kiislamu.

Wakatambulishwa kazi zinazofanywa na kituo cha turathi za Hilla, miongoni mwa tafiti, uandishi na nadwa, mwishoni wageni wakapewa zawadi ya chapisho la mwisho la jarida la Radu-Shamsi linaloandikwa na kituo hicho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: