Balozi ya Pakistani nchini Iraq Muheshimiwa Ahmadi Amjad Ali amesema kuwa, Zaidi ya watu laki tatu kutoka Pakistani huja kufanya ziara kwenye Ataba za Iraq kila mwaka.
Ameyasema hayo alipotembelea Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia kuisha kwa muda wake wa utumishi kama balozi wa Pakistani hapa Iraq.
Akasema kuwa “Wapakistani zaidi ya laki tatu huja kufanya ziara kwenye Ataba za Iraq kila mwaka”, akasema “Wapakistani laki moja na elfu themanini (180,000) waliingia nchini kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Hii ni ziara yangu ya mwisho nikiwa balozi wa Pakistani hapa Iraq, nimemaliza muda wangu wa kazi”.
Amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhudumia mazuwaru hasa wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu.