Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kuchimba kisima kipya katika nchi ya Tanzania kupitia mradi wa visima uitwao (Saaqi Atwasha Karbala) katika bara la Afrika.
Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Ugeni wa Markazi ukiongozwa na Sayyid Muslimu Aljabiri, umeanza kuchimba kisima namba (24) kupitia mradi wa (Saaqi Atwasha Karbala) unaofanywa kwenye nchi (13) za Afrika, kwa lengo la kuwapatia maji wakazi wa vijiji na miji yenye shida ya maji, huo ni miongoni mwa miradi yetu ya kibinaadamu katika bara la Afrika”.
Akaongeza kuwa “Visima vilivyopo kwenye Kijiji hicho vinauza maji, Markazi imeamua kuchimba kisima kwa lengo la kugawa maji bule chini ya baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), nacho kitakuwa kisima cha kwanza kugawa maji bure kwa wakazi wa Kijiji hicho”.
Akasisitiza kuwa “Markazi inaendelea kufanya ratiba za kibinaadamu, kiimani na kidini, kupitia wawakilishi wake waliopo kwenye nchi tofauti za Afrika”.