Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imefanya mahafali ya wahitimu awamu ya nne katika wanafunzi wake.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mahafali ya wahitimu wa masomo ya Qur’ani katika mji wa Najafu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Leo Maahadi inafanya mahafali ya wahitimu wa awamu ya nne ya wanafunzi wa masomo ya Qur’ani baada ya miaka minne waliyokaa darasani wakifundishwa Qur’ani na maarifa ya Qur’ani sambamba na Mantiki, Fiqhi, Aqida na masomo ya hadithi”.

Akaongeza kuwa “Mahafali yamefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na qaswida ya kauthariyya iliyosomwa na mwanafunzi (bi Ruqayya Yahya), ikafuata ripoti kwa njia ya picha halafu ikafuata qaswida ya (tutakusomesha hautasahau) kutoka kwa kikundi cha Nab’ul-Juud”.

Akaendelea kusema “Mwisho wa mahafali hiyo wahitimu wakapewa vyeti na zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: