Kitengo cha utalii wa kidini kimeandaa gari (43) kwa ajili ya kubeba wanafunzi Kwenda mkoani Karbala kushiriki kwenye mahafali ya wahitimu (mabinti wa Alkafeel) awamu ya sita.
Makamo rais wa kitengo cha utalii wa kidini Sayyid Ahmadi Shakiri Hashim amesema “Kitengo kimeandaa gari zitakazobeba washiriki kutoka mikoa sita Kwenda Karbala kwenye mahafali ya mabindi inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na watarudishwa kwenye mikoa yao baada ya mahafali”.
Akaongeza kuwa “Mikoa inayotoa washiriki ni, Karbala wanafunzi (250), Najafu wanafunzi (350), Kirkuuk wanafunzi (205) Diyala wanafunzi (55) Nainawa wanafunzi (65) na Swalahu Dini wanafunzi (50)”.
Atabatu Abbasiyya hufanya mahafali za wahitimu kila mwaka, mwaka huu itafanywa kwa siku mbili tarehe tisa na kumi za mwezi huu wa kumi na moja, nayo ndio mahafali kubwa zaidi yenye vipengele tofauti, hakika mahafali hii hujenga msingi bora wa kiroho kwa wahitimu na safari yao ya maisha ya kazi huanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).