Kitengo cha habari kinajadiliana na watumishi wa tawi la wanawake kuhusu namna ya kuripoti mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu.

Kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimejadiliana na watumishi wa idara ya wanawake kuhusu namna ya kuripoti mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq (Mabinti wa Alkafeel awamu ya sita).

Kamati inayosimamia mahafali hiyo, idhaa ya Alkafeel na maktaba ya Ummul-Banina (a.s) wamekubaliana namna bora ya kuripoti mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu, pamoja na kufanya mahujiano maalum na washiriki wa mahafali hiyo.

Kikao hicho kinakusudia kuhakikisha mahafali inakuwa na ufanisi mkubwa.

Atabatu Abbasiyya inafanya mahafali ya (Mabinti wa Alkafeel) itakayodumu kwa muda wa siku mbili, nayo ni miongoni mwa mahafali kubwa zaidi yenye vipengele tofauti kwa lengo la kumjenga mshiriki kiimani katika Maisha ya kazi ambayo huanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: