Mahafali hiyo inasimamiwa na idara ya shule za wasichana Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Kutokana na nuru ya Fatuma tunaangazia ulimwengu) ndani ya majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ushiriki wa zaidi ya wahitimu (1000) kutoka mikoa ya katikati ya Iraq, kusini na nje ya nchi.
Mahafali imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Maryam Ihsaan kutoka Maahadi ya Alkafeel chini ya Ataba tukufu katika mji wa Najafu, ikafuatiwa na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na (Lahnul-Ibaa), sambamba na kuonyesha kusimama pamoja na mashahidi wa Gaza na raia wa Palestina.
Mahafali imepampwa na ujumbe kutoka kwa kiongozi wa idara bibi Bushra Kinani, aliyeanza kwa kuwakaribisha wanafunzi wanaoshiriki kwenye mahafali hii, hususan waliotoka nje ya nchi (Kuwait, Baharain, Saudia, Oman, Lebanon na Iran).
Siku ya kwanza imekuwa na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni tukio la kiibada, mihadhara ya kimaadili na kitamaduni, igizo lisemalo (Ukuta wa mafanikio), qaswida za mashindano sambamba na ugawaji wa zawadi.
Mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu (Mabinti wa Alkafeel awamu ya sita) ni miongoni mwa mahali kubwa inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, inamchango mkubwa wa kuwajenga wahitimu kiimani, kwani huanza maisha yao ya kazi ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).