Ameyasema hayo kwenye ujumbe aliotoa mbele ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq (Mabinti wa Alkafeel) awamu ya sita, katika hafla inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Ulimwengu unaangaziwa kutokana na nuru ya Fatuma -a.s-).
Sayyid Swafi amesema “Nyie wote ni mradi wa familia, familia ndio mbegu ya kwanza katika jamii na baadhi ya watu wanataka kuharibu dhana hiyo na kuongea mambo yasiyokuwa na misingi ya kimaadili, maana halisi ya familia ni mume, mke na watoto, hakuna sehemu yeyote katika sheria inayokubali kuwa familia inaweza kuundwa na mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke”.
Akaondeza kuwa “Leo mmeingiza furaha katika nafsi zetu na mmeingiza furaha kwa kila mtu huru anayewatazama mabinti zetu mkitembea katika ardhi hii takatifu mkuwa mmevaa hijabu kamili na kuitangazia dunia kuwa mmemaliza hatua ya kujiandaa na vita sasa mnaingia hatua ya mapambano, hatua ya kufanya kazi”.
Akaendelea kusema: “Kupitia mahafali hii tunapenda kusisitiza kuwa misingi ya haki haitakufa na lazima ibaki, nyie kwa vazi hili tukufu lazima muendelee kusimamia na kulinda maadili mema na kupambana na mmomonyoko wa maadili unaojitokeza”.
Sayyid Swafi amewapongeza wahitimu kwa kufika hatua hiyo muhimu, pamoja na kupongeza wazazi na walezi wao kwa kazi kubwa waliyofanya kwa mabinti hao, ya kuwasimamia hatua baada ya hatua bila kusahau viongozi wa shule walizo soma na walimu kwa kazi nzuri ya kuwalea na kuwapa elimu”.
Mahafali hii imehudhuriwa na zaidi ya wanafunzi (2000) kutoka vyuo vikuu tofauti, kuanzia katikati ya Iraq, kusini, kaskazini na nchini Jirani, Kuwait, Saudia, Baharai, Oman, Iran, na Lebanon.
Hii ni miongoni mwa mahafali kubwa ambazo hufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, nayo husaidia kuwajenga wanafunzi kiroho na kuwafanya waanze ukurasa wa Maisha ya kazi wakiwa Jirani na kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).