Kitengo cha habari na utamaduni kimefanya Majlisi ya usomaji wa Qur’ani nchini Tanzania.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya Majlisi ya usomaji wa Qur’ani katika kitongoji cha Mbande nchini Tanzania.

Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema: “Ugeni kutoka Markazi katika bara la Afrika, umeratibu Majlisi ya usomaji wa Qur’ani katika kitongoji cha Mbande chini ya ushiriki wa wasomaji wakubwa wa Qur’ani na tajwidi”.

Akaongeza kuwa “Ugeni wa Markazi unaendelea kufanya harakati mbalimbali katika bara la Afrika, kwa lengo la kushajihisha watu kuisoma Qur’ani tukufu na kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.

Kiongozi wa ugeni huo nchini Tanzania Sayyid Muslim Aljabiri amesema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu ni sehemu ya mradi wa Markazi unaolenga kufundisha Qur’ani, Aqida na mambo ya kibinaadamu katika bara la Afrika”.

Akaongeza kuwa “Kikao hicho kilikuwa na wasomaji watatu na washindani watatu, kimehudhuriwa na watu wengi miongoni mwa wadau wa Qur’ani pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za kidini, Majlisi ikahitimishwa kwa kupata chakula kilichotokana na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: