Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya imewapa mtihani wanafunzi wake katika somo ya Hukumu za tajwidi.
Mkuu wa Maahadi tawi la Baabil bibi Alqat Suhail amesema “Maahadi imetoa mtihani wa somo la hukumu za tajwidi baada ya washiriki kimaliza masomo ya hukumu za usomaji, kwa lengo la kuangalia kiwango chao katika kuzielewa hukumu za usomaji na kuzifanyia kazi wakati wa kusoma Qur’ani tukufu”.
Akaongeza kuwa “Watahiniwa walikuwa (43) wanafunzi wenye umri tofauti na viwango tofauti vya elimu”.
Maahadi huandaa semina za Qur’ani, warsha na hutoa mihadhara kwa wanafunzi kwa lengo la kukuza vipaji vyao na kuwapa elimu itakayowasaidia katika uhai wao.