Majmaa-Ilmi inaendelea kutambulisha shindano la (Utafiti bora wa kuhitimu Qur’ani).

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea kutambulisha shindano la (Utafiti bora wa kuhitimu Qur’ani).

Shindano linasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa, nalo ni sehemu ya miradi ya Qur’ani kwenye vyuo vikuu awamu ya nne mwaka (2023 – 2024m), linalenga wanafunzi wa masomo ya Qur’ani katika vyuo vikuu.

Mradi unalenga chuo cha Shekhe Tusi, kitivo cha Fiqhi, chuo cha Imamu Swadiq (a.s) kwa kuwatambulisha wanafunzi shindano hilo litakalo simamiwa na Maahadi, sambamba na zawadi zilizo andaliwa kwa washindi sita wa mwanzo.

Mradi huo unahusisha ufanyaji wa nadwa za Qur’ani kwenye vyuo vikuu na Maahadi, kufanya mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani, kufanya maonyesho ya Qur’ani awamu ya pili, kufanya shindano la Qur’ani kwa njia ya mtandao awamu ya tatu, semina za kufundisha usomaji sahihi na kanuni za tajwidi, kuwajengea uwezo walimu wa vyuo vikuu, safari za kidini na mengineyo yanayolenga kuhamasisha usomaji wa Qur’ani tukufu katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: