Program ya watumishi imeshuhudia muhadhara wa kitamaduni na kiitikadi.

Program inayohusu watumishi, inayo endeshwa na kamati ya program za Atabatu Abbasiyya na kutekelezwa na kitengo cha maendelep endelevu, imeshuhudia muhadhara wa kitamaduni na kiitikadi.

Mkufunzi Sayyid Jawadi Twawiil amesema “Mihadhara ya kitamaduni na kiitikadi imelenga kujenga uwelewa wa kitu gani ufanye kitakacho akisi tabia nzuri na uwelewa wa madhehebu” akabainisha kuwa “Tumejikita kwenye nafasi ya Hauza na changamoto zake sambamba na kuangalia namna ya kupambana nazo”.

Akaongeza kuwa “Baada ya kutolewa muhadhara ukafunguliwa mlango wa maswali na majibu kutoka kwa watumishi, wamejadili mambo mbalimbali katika sheria ya kiislamu”.

Muhadhara huo ni sehemu ya muendelezo wa mihadhara tofauti na nadwa ambazo zimekuwa zikifanywa na kitengo cha maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: