Muheshimiwa katibu mkuu amefuatana na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, ambao ni Sayyid Kaadhim Abaadah, Sayyid Jawadi Hasanawi, Sayyid Muhammad Ashqari na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh.
Msimsmizi mkuu wa mradi Muhandisi Haidari Shakiri Rashidi amesema “Ziara ya kamati ya wizara ya afya iliyofanywa hivi karibuni imetupa ruhusa ya kusajili mradi na kutengeneza vifaa-tiba tofauti, pamoja na vifaa vya ujenzi, kemikali, umeme na vinginevyo”.
Akaongeza kuwa “Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu wametembelea mradi wa kutengeneza vifaa-tiba na kuangalia aina zinazo tengenezwa sambamba na vitu vya lazima vinavyo hitajika kwenye mradi huo”.
Akaendelea kusema “Mradi huo umepasishwa na wizara ya afya na ilisema kuwa ni mradi bora zaidi wa vifaa-tiba nchini Iraq. Kwani unatengeneza dawa nzuri zinazoendana na maendeleo ya kisasa kwenye sekta hiyo”.
Kiwanda cha Aljuud kinacho tengeneza vifaa-tiba, ni moja ya miradi mikubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa raia wa Iraq, kwa lengo la kupunguza uhaba wa vifaa-tiba na kuendeleza viwanda vya dawa hapa nchini.