Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa nadwa kuhusu maadili ya udaktari kwa wanafunzi wa kitivo cha uuguzi kwenye chuo kikuu cha Karbala.
Shekhe Muhammad Kuraitwi amesema kuwa “Nadwa hii ni sehemu ya ratiba inayotekelezwa na idara ya Tablighi katika kitengo cha Dini, inahusisha ufanyaji wa nadwa na utoaji wa mihadhara kwenye vyuo vikuu na Maahadi za Iraq, inalenga kuimarisha mahusiano baina ya taasisi za kidini na kisekula sambamba na kuangalia namna ya kutatua changamoto za wanafunzi”.
Akaongeza kuwa “Nadwa imedumu kwa muda wa saa moja na nusu, imehusisha muhadhara wa maadili ya madaktari na watumishi wa sekta ya afya pamoja na maadili ya kifiqhi kwa wanafunzi”.
Nadwa imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi, wameuliza maswali na kutoa maoni mbalimbali.