Kitengo cha utalii: Kimeandaa gari 60 kwa ajili ya kubeba wanafunzi 1100 watakaoshiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa chuo.

Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa, Gari 60 zimeandaliwa kwa ajili ya kubeba wanafunzi 1100 watakao shiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq (Juu ya uongofu wa mwezi awamu ya tatu).

Makamo rais wa kitengo Sayyid Ahmadi Shakiri Hashim amesema “Kitengo kimeandaa gari (60) kwa ajili ya kubeba washiriki wa mahafali ya wahitimu wa chuo”.

Akaongeza kuwa “Tunajukumu la kubeba wanafunzi karibu 1100 kutoka mkoa wa Mosul, Ambaar, Swalahu-Dini, Najafu, Baabil na Diyala, kuwaleta katika mji wa Karbala na kuwarudisha baada ya mahafali”.

Atabatu Abbasiyya hufanya mahafali ya wahitimu tarehe kumi na saba mwezi wa kumi na moja kila mwaka, hupambwa na vipengele tofauti vinavyo lenga kuwapongeza na kuwajenga kiroho wahitimu.

Atabatu Abbasiyya tukufu itafanya mahafali kubwa ya wahitimu, ambapo wanatarajiwa kushiriki wahitimu kutoka mikoa tofauti ya Iraq, hii ni sehemu ya kupongeza safari yao ya masomo na kuihitimisha wakiwa mbele ya malalo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: