Atabatu Abbasiyya inaendeleza nadwa maalum katika (Kuangazia tamko la Marjaa-Dini mkuu kuhusu swala la Palestina).
Nadwa hizo zinasimamiwa na kitengo cha maendeleo endelevu katika Ataba tukufu.
Mhadhiri na mtafini bwana Hassan Ali Aljawaadi amesema “Muhadhara umejikita katika kueleza msimamo wa Marjaa-Dini mkuu kuhusu swala la Palestina, kuanzia mwaka (1932) hadi (2023) hususan msimamo wa hivi karibuni wa Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umeangazia msimamo wenye vipengele vingi kuhusu swala la Palestina, kuanzia utoaji wa takwimu na vielelezo vya kudumu kwa kizazi na kizazi kuhusu swala la ubinaadamu”.
Akabainisha kuwa “Atabatu Abbasiyya itaendelea kufanya nadwa katika wiki zijazo kubainisha haki ya raia wa Palestina, chini ya uadui na maaafa makubwa wanayopata”.