Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema kuwa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq inakusanya watu wa Dini na tamaduni tofauti chini ya bendera ya Iraq.
Akaendelea kusema “Mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu inawakusanya raia wote chini ya bendera ya Iraq na Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya inafanya mahafali ya wahitimu yenye anuani isemayo (Juu ya uongofu wa mwezi awanu ya tatu), kuna jumla ya wahitimu (2500) kutoka vyuo (44) mikoa (15) kuanzia mikoa ya kaskazini hadi kusini mwa Iraq”.
Akaendelea kusema “Atabatu Abbasiyya inatoa ujumbe kwa walimwengu kuwa Mwanafunzi wa Iraq anahadhi kubwa na ni wakujivunia, kwani ndiye mbegu ya kujenga taifa, jamii, uchumi na mengineyo”.
Atabatu Abbasiyya hufanya mahafali kwa wahitimu wa vyuo vikuu, ambayo huwa ni mfano mzuri kwa vyuo vyote vya Iraq.