Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza majina ya washindi wa shindano maalum lililofanywa kufuatia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s).
Sharti la kupokea zawadi , mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mazazi ya bibi Zainabu (a.s), itakayofanywa katika eneo la mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi kesho siku ya Jumapili (19/11/2023m) sawa na mwezi (4 Jamadal-Uula 1445h), iwapo mshindi atakuwa na dharura ya kushindwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa aende kwenye kitengo cha mali katika Atababatu Abbasiyya ndani ya siku nne toka kutangazwa kwa matokeo, akiwa na kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria (Paspoti).