Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa mji wa Kaduna kaskazini ya Naijeria.
Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Markazi iliandaa program iliyohitimishwa kwa usomaji wa Qur’ani tukufu katika mji wa Kaduna nchini Naijeria, ilihudhuriwa na wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Hafla imesimamiwa na muwakilishi wa Markazi katika mji huo, inalenga kueneza utamaduni wa kusoma na kuhifadhi Qur’ani tukufu katika jamii ya waafrika, sambamba na kushajihisha vijana na wanafunzi kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Akabainisha kuwa “Program ya kusoma Qur’ani ni sehemu ya muendelezo wa program za kitablighi zinazo simamiwa na Markazi katika bara la Afrika”.