Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kikao na watumishi wa jarida la Mtume wetu (s.a.w.w) kwa ajili ya kuangalia maendeleo yake kielimu.
Mkuu wa Daru RasuuluL-A’adham Dokta Aadil Nadhiir amesema “Tumefanya kikao na kamati ya wahariri wa jarida la Mtume wetu, kujadili namna ya kuwapata watafiti na wabobezi watakao Andika kuhusu Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.
Akaongeza kuwa “Katika kikao hicho tumejadili utukufu wa Mtume (s.a.w.w), tukaangalia idadi ya majarida yanayo Andika kuhusu Mtume na kiwango cha elimu inayotolewa na majarida hayo”.
Akaendelea kusema “Kikao kimejikita katika kuangalia namna ya kuongeza kiwango cha elimu inayotolewa na majarida, tumekubaliana kufanya warsha kwenye vyuo vikuu vya Iraq”.
Jarida la Mtume wetu linatolewa na Daru Rasulul-A’adham (s.a.w.w) chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lugha la kiarabu, kiengereza na kifarsi.