Makamo rais wa kitengo Muhandisi Kadhim Swalehe Mahadi amesema “Watumishi wa kitengo chetu wamepamba eneo la katikati ya haram ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuweka Zaidi ya vitambaa (57) vyenye ukubwa tofauti”.
Akaongeza kuwa “Vitambaa vimewekwa juu ya nguzo za taa na vimeandikwa maneno ya kupongeza mazazi ya Aqilah Twalibina bibi Zainabu (a.s)”.
Kitengo huwa kinaweka mazingira ya furaha katika tarehe za kumbukumbu za mazazi ya Maimamu watakasifu (a.s), ikiwa ni pamoja na kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s).