Rais wa kitengo hicho Sayyid Khaliil Hanuun amesema “Mapokezi haya ni moja ya shughuli zinazofanywa na Ataba tukufu katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mazazi haya matukufu”, akabainisha kuwa “Mazuwaru wamefurahia mapokezi mazuri wanayopewa na wameshukuru sana”.
Akaongeza kuwa “Watumishi wa malalo takatifu wamesimama kwenye milango ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kupokea mazuwaru kwa maneno mazuri na kuwapa pipi, sambamba na ugawaji wa vitambaa vilivyo andikwa maneno ya pongezi”.