Maadhimishoya kuzaliwa bibi Zainabu.. watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanafanya tukio la kiibada.

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wamefanya tukio la kiibada ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s).

Tukio hilo limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha wimbo wa (Lahnul-Ibaa), mbele ya idadi kubwa ya marais wa vitengo na mazuwaru watukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tukio limepambwa na qaswida na mashairi yanayohusu mazazi ya Hauraa (a.s) na kuhitimishwa kwa kugawa mauwa na halwa kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: