Maadhimisho yamefanywa katika eneo la vitalu vya Alkafeel kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Sayyid Muhammad Kaadhim kutoka kitengo cha maadhimisho amesema: “Atabatu Abbasiyya imefanya maadhimisho mengi katika mnasaba wa kuzaliwa bibi Zainabu (a.s), kwenye maadhimisho hayo yameongelewa mambo mengi kuhusu Maisha ya bibi Zainabu (a.s).
Akaongeza kuwa “Maadhimisho yalikuwa na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na uimbaji wa qaswida na mashairi yanayo muhusu bibi Zainabu (a.s)”.
Makamo kiongozi wa vitalu vya Alkafeel Muhandisi Dhiyabu Ahmadi Sharifi amesema “Maadhimisho yaliyofanywa kwenye eneo hili yamelenga familia za watu wa Karbala na mazuwaru watukufu, yamepambwa na ugawaji wa zawadi na mauwa”.
Akaongeza kuwa “Wakati wa maadhimisho hayo, tumeeleza utukufu wa bibi Zainabu (a.s) na historia yake takatifu”.
















