Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimeanza kutengeneza vivuko kwenye Barabara zinazoelekea katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kimeanza kutekeleza mradi wa kuweka vivuko kwenye Barabara zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara ya mafundi Mhandisi Alaa Hamza amesema “Kitengo chetu kwa kushirikiana na kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi na miradi ya kihandisi, tumeanza kutekeleza mradi wa kutengeneza vivuko kwenye Barabara zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Mradi huo unafanywa kwenye Barabara ya Alqami, utaendelea pia kwenye Barabara ya Babu Qibla, Babu Baghdad na Barabara zingine”.

Akaendelea kusema “Lengo la mradi huu ni kudhibiti vyombe vinavyotembea ndani ya eneo la mji mkongwe, sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuweka mfumo rahisi wa kuvitambua vyombo hivto”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: