Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimehitimisha ratiba ya kuandaa washauri nasaha katika sekta ya familia na saikolojia.

Kiongozi wa kituo bibi Sara Alhafaar amesema “Program ilikuwa na mihadhara miwili iliyotolewa na mbobezi wa mambo ya familia na saikolojia Dokta Shaimaa Nasoro, muhadhara wa kwanza ameongea kuhusu (Utaratibu wa kutoa maamuzi na utatuzi wa migogoro) na muhadhara wa pili akaongea kuhusu (Jihadi na ufanisi wa vitendo)”.

Akaendelea kusema “Ratiba ikahitimishwa kwa kuwapa mtihani washiriki ili kupima uwezo wao kwa kuzingatia mafundisho ya Ahlulbait (a.s)”.

Kituo kinaendelea kutoa mafunzo tofauti kwa kutumia mbinu za kisasa, kwa lengo la kupata washauri nasaha bora watakao weza kutatua changamoto za familia na mambo ya kisaikolojia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: