Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anaangalia maendeleo ya kazi katika mradi wa ukanda wa kijani.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini ametembelea mradi wa ukanda wa kijani.

Rais wa kitengo cha ukanda wa kijani kibichi Sayyid Nasoro Husseini Mut’ibu amesema “Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na ujumbe aliofuatana nao, wametembelea mradi wa ukanda wa kijani na kuangalia maendeleo ya kazi kwenye maeneo zaidi ya kumi”.

Akaongeza kuwa “Muheshimiwa katibu mkuu amesisitiza kuwa mradi unatakiwa uwe wa kiuchumi na kimapumziko, utoe huduma kwa wakazi wa Karbala na mazuwaru”, akafafanua kuwa “Watumishi wa mradi wa ukanda wa kijani kibichi wameandaa zaidi ya maeneo (24) ambayo yapotayali kupokea familia za kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mut’ibu, wageni rasmi na wasiorasmi wanaendelea kuja kuangalia mradi wa ukanda wa kijani kibichi na mafanikio yaliyofikiwa na Atabatu Abbasiyya katika utunzaji wa mazingira.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: