Majmaa-Ilmi yaendesha kisomo cha Qur’ani katika mji wa Bagdad.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na semina za Qur’ani kwa mubalighina na walimu ndani ya jiji la Baghdad.

Ratiba hiyo husimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa.

Rais wa kitengo cha Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu Dokta Mushtaqu Ali amesema “Kufanya harakati za kitamaduni na kielimu hususan masomo ya Qur’ani katika mji mkuu wa Baghdad, unatokana na umuhimu wa mji huo pamoja na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya ya umuhimu wa kufundisha Qur’ani katika jamii ya waislamu, tunaendelea na ratiba ya Qur’ani kwa wanaoanza na walimu”.

Tambua kuwa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu hufanya program nyingi za Qur’ani kwenye maeneo tofauti ya mji wa Bagdhad, kwa lengo la kujenga utamaduni wa kushimakana na vizito viwili ndani ya Jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: