Kongamano hilo linafanywa kuanzia tarehe (23 – 24/11/2023m) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kongamano limehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya viongozi wa Ataba pamoja na wasomi na watafiti wa mambo ya maktaba kutoka ndani na nje ya nchi.
Kongamano limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Liith Al-ubaidi, iliyofuatiwa na wimbo wa (Lahnul-Ibaa).
Siku ya kwanza kutakuwa na ujumbe kutoka uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, ujumbe kutoka kamati kuu ya athari na turathi, ujumbe kutoka umoja wa makumbusho za kiarabu (ICOM), kisha itaonyeshwa filamu inayoelezea makumbusho ya Alkafeel, halafu utafuata ujumbe kutoka makumbusho ya Alkafeel, kisha utafuata ujumbe wa kamati ya elimu na ujumbe kutoka kwa wageni wakiarabu na kiajemi.
Aidha siku ya kwanza itakuwa na uwasilishaji wa mada za kielimu kutoka kwa watafiti wa kiarabu na kiajemi.
Kongamano limejikita katika kueleza mchango wa makumbusho katika kulinda utamaduni na kutangaza turathi kwenye mitandao ya kijamii, sambamba na kueleza nafasi ya makumbusho katika utaifa na utamaduni, mada zitakazo wasilishwa zina anuani zisemazo: Makumbusho na changamoto ya utamaduni, Nafasi ya makumbusho katika mkakati wa maendeleo endelevu, Ukarabati na nafasi yake katika kulinda mali-kale za makumbusho, Ujumbe wa makumbusho na nafasi yake katika utambulisho wa utamaduni.
Unawezo kushiriki kongamano kupitia jukwaa la (ZOOM) au kupitia link ifuatayo: https://alkafeel-edu-iq.zoom.us/j/95647956344