Kitengo cha maarifa kimefanya mkutano wa kujadili maudhui za jarida la turathi za Basra.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kikao cha kujadili maudhui za jarida la turathi za Basra.

Kikao hicho kimehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kituo cha turathi za Basra Shekhe Mudrik Hasuun, rais wa wahariri wa jarida Dokta Mahmudu Idani na Dokta Aamiri Saadi na baadhi ya wajumbe wa kamati ya wahariri, wamejadili maudhui na toleo la (16-17).

Wajumbe wameongea kuhusu maudhui na milango ya msigi katika jarida, sambamba na kupokea maoni tofauti kuhusu tafiti, maoni yote yatawasilishwa kwenye kamati ya elimu kwa uchunguzi zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: