Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imewapa mtihani walimu wa semina za Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya.
Msimamizi wa mtihani huo ni Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Majmaa.
Watahiniwa walikuwa (30), wameulizwa maswali ya kanuni za usomaji wa Qur’ani, matamshi sahihi ya herufi za Qur’ani, usomaji mzuri, sauti, naghma, ili kutambua uwezo walionao walimu.
Maswali yote yametokana na mada walizofundishwa wakati wa semina za kuwajengea uwezo, hakika mtihani ni njia nzuri ya kutambua uwezo wao na udhaifu wao.