Kuanza msimu wa huzuni za Fatwimiyya katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu umeanza kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Maombolezo hayo yanasimamiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kuanzia tarehe (10 Jamadal-Uula hadi 3 Jamadal-Aakhar).

Hafla ya ufunguzi wa maombolezo hayo imehudhuriwa na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo na wenye mawakibu Husseiniyya.

Rais wa kitengo Sayyid Aqiil Yasiriy amesema “Msimu wa huzuni za Fatwimiyya hufanywa kila mwaka katika kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili, huwa na vipengele vingi ikiwa ni pamoja na kueleza historia yake takatifu”.

Akaongeza kuwa “Ratiba ya maombolezo huhusisha igizo kuhusu Maisha ya bibi Zaharaa (a.s) na tukio la kuvamiwa nyumba yake, picha ya nyumba ya huzuni aliyojengewa na kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) na igizo lingine la mazishi yake (a.s)”.

Akaendelea kusema “Hushiriki mawakibu Husseiniyya, kikosi cha Abbasi, kitengo cha malezi na elimu ya juu, kitengo cha Habari kwa ajili ya kuikumbusha dunia yaliyotokea kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na ukubwa wa tukio hili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: