Makamo rais wa kitengo kinachosimamia haram tukufu Shekhe Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Ataba tukufu imeweka mazingira ya huzuni kufuatia kumbukumbu ya kifo cha bibi Fatuma (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Majlisi kadhaa zimefanywa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na nje ya mji wa Karbala katika mkoa wa Baghdad, Diyala, Mosul, Majlisi hizo zinafanywa kwa kushirikiana na kitengo cha Dini, kwa lengo la kuongea dhulma alizofanyiwa bibi Zaharaa (a.s)”.
Akabainisha kuwa “Haram tukufu imekamilisha uwekaji wa mapambo meusi na mabango yaliyoandikwa ujumbe unaohusu dhulma alizofanyiwa bibi Zaharaa (a.s), akasema “Majlisi za kuomboleza zitaendelea kwa siku kadhaa”.