Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa muhadhara wenye anuani isemayo (Nguvu ya mtu alama na dalili) kwa washiriki wa kongamano la mabinti wa Hauraa Zainabu (a.s).
Mkuu wa kituo bibi Sara Haraar amesema “Muhadhara ni sehemu ya mradi wa (Wabebaji wa ujumbe wa Zainabiyya) unaosimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, unaojikita katika kuimarisha hutuba za maelekezo ya kinafsi kwa wanawake”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umetolewa na bibi Sundusi Muhammad kwa washiriki wa kongamano la mabinti wa Hauraa Zaianabu (a.s), ameongea namna ya kuimarisha nguvu za utu na jinsi ya kujiendeleza”.
Akaendelea kusema “Kituo cha utamaduni wa familia hutoa huduma za ushauri kwa wanafamilia, kwa lengo la kuimarisha ustawi wa familia za raia wa Iraq kwa kufuata misingi ya Ahlulbait (a.s)”.