Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.
Majlisi hiyo imehudhuriwa na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha akapanda mimbari Shekhe Imadu Naasir.
Naasir amesema “Katika Majlisi ya leo tumejikumbusha Maisha ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kubainisha dhulma alizofanyiwa na maadui wa Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kufanya Majlisi za Husseiniyya katika matukio ya Ahlulbait (a.s) ni sehemu ya kupata mazingatio katika Maisha yao matukufu”.
Majlisi ikahitimishwa kwa qaswida ya kuomboleza iliyoamsha hisia za husuni na majonzi katika nyoyo za waumini.
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza matukio ya Ahlulbait (a.s) yenye vipengele tofauti.