Atabatu Abbasiyya inapokea mawakibu za kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea mawakibu za maombolezo ya Fatwimiyya, katika kumbukizi ya kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.

Mawakibu za kuomboleza zinakuja kutoa pole kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Mawakibu za zanjiil na matam zinakuja kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha zinatoka na kupita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) ambako zinafanya Majlisi ya kuomboleza.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kupokea mawakibu za kuomboleza, sambamba na kuandaa mimbari za kutolea mihadhara ya kidini, aidha imeandaa Majlisi katika maeneo tofauti kwa ajili ya kueleza utukifu wa bibi Fatuma (a.s) na yaliyomsibu baada ya kifo cha baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: