Siku ya pili… idara ya wahadhiri wa Husseiniyya inaendelea kuhuisha maombolezo ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya kitengo cha wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa siku ya pili mfululizo.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi amesema “Kwa kushirikiana na kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s), tunaendelea kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa siku ya pili mfululizo”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa ziara ya bibi Zaharaa (a.s), ikafuatiwa na igizo la Maisha ya bibi Fatuma (a.s) lenye anuani isemayo (Fatuma ni hoja na mazingatio)”.

Akaendelea kusema “Idara ilionyesha picha ya kushambuliwa nyumba ya mbora wa wanawake wa ulimwenguni, iliyopambwa na qaswida za kuomboleza sambamba na kutoa pole kwa Imamu Mahadi (a.f)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: