Kwa mujibu wa riwaya ya pili.. Idara ya maelekezo ya kidini inafanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Swidiqatu-Twahirah.

Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili, kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Adhraa Shami amesema “Majlisi imefanywa Jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) ndani ya Ataba tukufu na itadumu kwa muda wa siku tatu”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na kisomo cha ziara ya bibi Zaharaa (a.s) mbele ya kundi kubwa la mazuwaru”.

Akaendelea kusema “Kisha mmoja wa wahadhiri akatoa muhadhara kuhusu dhulma alizofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) na umuhimu wa kufuata mwenendo wake mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: