Idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.
Sayyid Badri Mamitha mmoja wa wajumbe wa idara hiyo amesema “Idara imefanya Majlisi ya kuomboleza na kutaja dhulma alizofanyiwa mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imefanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na muhadhara kuhusu nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) mbele ya Mtume (s.a.w.w) na maudhi aliyopata wakati akitetea ujumbe wa Mtume na Uimamu, hakika alitetea ujumbe wa baba yake na Uimamu wa mume wake”.
Akaendelea kusema “Majlisi imehitimishwa kwa kusoma Qaswida na tenzi za kuomboleza, zilizoamsha hisia za majonzi na huzuni katika nyoyo za waumini”.
Atabatu Abbasiyya inaratiba maalum ya kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) yenye vipengele vingi.