Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel kimesaini makubaliano ya kushirikiana na chuo kikuu cha Baghdad kwenye sekta ya elimu na tafiti.
Utiaji wa saini umetokana na ziara ya wajumbe wa chuo iliyo ongozwa na Dokta Karim Ghanimi kutoka chuo kikuu cha Baghdad, ambao wamepokewa na mkuu wa kitivo cha udaktari Dokta Raghad Hashimi na baadhi ya viongozi wa chuo.
Makubaliano waliyosaini yanahimiza kushirikiana kwenye mambo yote ya kielimu chini ya kanuni na muongozo wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
Ugeni umetembelea maabara na kuangalia vifaa vilivyopo katika kitivo cha udaktari wa meno.