Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s).
Sayyid Badri Mamitha kutoka idara ya Masayyid wanaohudumia Atabatu Abbasiyya amesema “Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.
Akaongeza kuwa “Maukibu imeanzia katika Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuelekea haram ya Imamu Hussein (a.s), ambako wameenda kumpa pole kwa kufiwa na mama yake Swadiqatu-Twahirah (a.s)”.
Watumishi wa Ataba mbili huadhimisha matukio yote yanayohusu Ahlulbait (a.s), na wameshiriki kwa pamoja na waumini wengine katika kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w).