Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umeshuhudia kitengo cha kiibada kufuatia kuomboleza kifo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.
Mmoja wa watumishi wa kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aal-Mamitha amesema “Tukio la kiibada hufanywa siku ya Jumatatu na Alkhamisi ya kila wiki, huanza kwa kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi huku wakiwa wamesimama kwa mistari mbele ya kaburi takatifu, ikifuatiwa na wimbo wa (Lahnul-Ibaa)”.
Akaongeza kuwa “Tukio limehusisha kuomboleza kifo cha mmbora wa wanawake bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kusoma qaswida na tenzi za kuomboleza”.
Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s) kwa kuandaa ratiba maalum yenye vipengele vingi.