Ameyasema hayo alipompokea muwakilishi wa idara ya wizara ya ujenzi na makazi Sayyid Jadarji na wakaongea kuhusu sekta ya kilimo.
Sayyid Swafi amesema, Kilimo ni mradi mkubwa unaopunguza tatizo la ukosefu wa ajira, akasisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria za Iraq wakati wa kutekeleza mradi wowote.
Akasisitiza umuhimu wa sekta ya kilimo na kunufaika na ardhi katika maendeleo ya taifa na ustawi wa nchi.
Muheshimiwa Matiin Jadarji amesema “Tumefanikiwa kumtembelea kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na tumeongea kuhusu miradi inayofanywa na Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa “Sayyid Swafi ameonyesha utayali wa kusaidia mradi wowote unaolenga kumtumikia raia wa Iraq na kuendeleza taifa”, akasisitiza “Atabatu Abbasiyya inafanya miradi tofauti kwa ajili ya ustawi wa taifa”.